The Weather Channel

The Weather Channel kama Mtoa Huduma za Hali ya Hewa

Hujambo! The Weather Channel inamiliki na huchapisha tovuti ya weather.com, programu ya mkononi ya The Weather Channel na programu nyingine zinazohusiana na hali ya hewa. Lakini wakati mwingine, The Weather Channel hutoa taarifa zetu za hali ya hewa kwa kampuni nyingine ambazo zinawasilisha taarifa hizo za hali ya hewa kwako katika tovuti zao binafsi, programu za mkononi na [rogramu nyingine. Ukurasa huu unaelezea jinsi The Weather Channel hutumia data yako katika hali hizo mahususi. Kwa maswali mengine yote kuhusu ukusanyaji wa data binafsi, matumizi na/au kushiriki kutumia tovuti ya kampuni nyingine, programu ya mkononi au programu nyingine, tafadhali pitia sera ya faragha ya kampuni hiyo.

Mifumo ya usambazaji data ya The Weather Channel inaweza kutoa taarifa za hali ya hewa kiotomatiki za eneo husika ikiwa tutapewa eneo husika katika miundo michache inayotambulika kama vile misimbo ya eneo, majina ya miji na misimbo ya jiografia (latitudo/longitudo). Tunaweza kupewa data ya eneo kiotomatiki na programu unayotumia, au unaweza kuandika na kuchagua eneo kupitia utafutaji, kutegemea na jinsi kampuni nyingine imeunda tovuti au programu yake. Kwa njia yoyote, The Weather Channel itatumia data ya eneo kwa madhumuni tu ya kutoa taarifa ya hali ya hewa ya eneo hilo kwako. (Tafadhali fahamu kwamba hii haimaanishi kuwa tovuti au programu ya kampuni nyingine haitumii data yako ya eneo kwa madhumuni mengine, hivyo soma sera ya faragha ya kampuni nyingine kwa maelezo zaidi.) Inapohitajika, mfumo wa uendeshaji(OS), kivinjari, au programu ya mkononi unayotumia inaweza kuomba ruhusa ya kutumia data yako ya eneo au kukuonyesha ilani kwamba data yako ya eneo inatumika. Hili likitendeka itategemea OS, kivinjari, au programu unayotumia na ikiwa ulitoa ruhusa awali au uliona ilani mapema. Tafadhali fahamu kwamba kwa sababu The Weather Channel haimiliki, kudhibiti wala kudumisha OS, kivinjari wala programu unayotumia, hatuwezi kudhibiti ikiwa na wakati unapokea ilani wala kuomba ruhusa ya kutumia eneo lako.

Kama vile tu watu hawawezi kutumia barua bila anwani za barua, vifaa kwenye intaneti haviwezi kuwasiliana bila anwani za IP. Kwa sababu ya hili, tovuti au programu ya tovuti nyingine hutumia anwani ya IP ili tuweze kutoa taarifa za hali ya hewa hadi kwenye kifaa chako. Kampuni nyingine inaweza kuwasiliana na The Weather Channelkwa kutumia anwani ya IP iliyotengewa kifaa chako wakati huo au anwani ya IP kwa ajili ya mifumo yao ya ndani. Kwa njia yoyote, The Weather Channel itatumia anwani ya IP kwa madhumuni tu ya kukupa taarifa ya hali ya hewa.

Huenda unashangaa,“Je, Sera ya Faragha ya The Weather Channel inatumika kwangu wakati gani?” Sera ya Faragha ya The Weather Channel inatumika tu wakati mtumiaji anatembelea tovuti, programu ya mkononi, programu nyingine iliyochapishwa na kumilikiwa na The Weather Channel.